Katika mwaka wa fedha 2023/2024,
Wakala ulipanga kutekeleza jumla ya Miradi 1,546
katika mikoa 25 nchini,
inayogharimu kiasi cha Tshs 500,342,398,033.25. Miradi hiyo inategemewa
kuhudumia watu wapatao 2,274,193 katika vijiji 844.
Katika kipindi cha nusu mwaka
wa fedha 2023/2024, hadi kufikia Desemba 31, 2023 jumla ya miradi 374 iliyogharimu kiasi cha Tshs 128,177,655,882
ilikuwa imekamilika. RUWASA inaendelea na utekelezaji wa miradi 1,172 iliyobakia
ili kutimiza adhma ya serikali ya kutoa
huduma ya uhakika ya Maji Safi na Salama vijijini.