Dira
Kuwa na jamii inayopata
huduma ya majisafi, salama na usafi wa mazingira vijijini kwa maendeleo ya
kijamii na kiuchumi.
Dhamira
Kutoa na kusimamia huduma
ya majisafi na salama na kuhamasisha usafi wa mazingira kwa jamii iishio
vijijini kwa ushirikiano, weledi na kwa gharama nafuu.
Tunu za RUWASA
- Ushirikiano: Kufanya kazi kwa
ushirikiano ili kuhakikisha jamii iishio vijijini inapata huduma ya
majisafi na salama;
- Utu: Kuzingatia utu
katika utendaji kazi kwa kuwajali na kuwathamini wateja na wadau wetu;
- Uwazi: Kutoa huduma
kwa wateja wetu kwa kuzingatia ukweli na uwazi;
- Taaluma na Weledi: Kutekeleza
majukumu kwa kuzingatia taaluma na weledi ili kuwa na miradi yenye ubora
na endelevu;
- Uadilifu: Kufanya kazi
kwa kuzingatia uadilifu
- Kuwajibika: Kutekeleza
majukumu kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu
- Kujali Mteja: Kuhakikisha
mteja anapewa kipaumbele katika utoaji wa huduma
- Ubunifu: Kuthamini mawazo
mapya katika utendaji kazi