Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

WAKALA WA MAJI NA USAFI WA MAZINGIRA VIJIJINI

"Maji Bombani"

Masharti ya Matumizi

Kanuni zifuatazo zinahusu matumizi yote ya tovuti, mifumo na huduma za tovuti zilizo ndani ya tovuti hii na taarifa zote juu ya mifumo na huduma za Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA).


Huduma hutolewa kwa sharti la mtumiaji kukubali maboresho yote ya sheria na masharti yaliyomo katika sheria nyingine za uendeshaji, sera, notisi, miongozo na taratibu zitakazotangazwa na RUWASA mara kwa mara.


Aidha, tunaweza kurekebisha tovuti hii na huduma zetu   na kwamba kanuni hizi zitaendelea kuhusika panapo mabadiliko.


Tafadhali soma makubaliano haya kwa uangalifu kabla ya kutumia huduma zetu. Kwa kutumia sehemu yoyote ya huduma zetu, unakubali kufungamana na kanuni na masharti ya makubaliano haya. Ikiwa haukubaliani na kanuni na masharti yote ya makubaliano haya, hautaweza kutumia sehemu yoyote ya huduma hii.