Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

WAKALA WA MAJI NA USAFI WA MAZINGIRA VIJIJINI

"Maji Bombani"

Rais Mstaafu Kikwete asisitiza elimu ya uvunaji maji ya mvua

Rais Mstaafu Kikwete asisitiza elimu ya uvunaji maji ya mvua

Rais Mstaafu wa awamu ya nne Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete ametembelea banda la Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijiijini (RUWASA) lililopo katika maonesho ya Mkutano wa Kimataifa wa Wadau wa Maji unaojulikana kama International Maji Scientific Conference 2024 unaoendelea katika Ukumbi wa Mlimani CIty Dar es Salaam kwa siku tatu kuanzia tarehe 31 Januari, 2024.


Baada ya kupatiwa maelezo kuhusu RUWASA na kazi zake pamoja na kuoneshwa teknolojia ya kuvuna maji ya mvua ambayo RUWASA imekuwa ikiwaelimisha wakazi hususani wa maeneo ya vijijini kuitumia, Mstaafu Kikwete amesisistiza kutolewa elimu zaidi ikiwa ni pamoja na kuwaelimisha wadau hao jinsi ya kuhifadhi maji wanayoyavuna na gharama za madawa yanayotumika kuyatibu ili yasiharibike.