Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

WAKALA WA MAJI NA USAFI WA MAZINGIRA VIJIJINI

"Maji Bombani"

Programu ya Malipo kwa Matokeo (PforR)

Programu ya Malipo kwa Matokeo (PforR) ni mpango wa Benki ya Dunia ulioanza tarehe 15, Julai 2019 kama programu ndogo chini ya Programu Endelevu ya Usambazaji wa Maji Vijijini na Usafi wa Mazingira (SRWSP). Lengo kuu la Programu ya Malipo kwa Matokeo ni kuchochea mafanikio ya SRWSP kupitia uwezeshaji ambao husababishwa na idadi ya viashiria vinavyohusiana na malipo (DLIs). Viashiria hivyo hupima na kutuza Wilaya kwa kufikia malengo yaliyopangwa kwa mwaka. SRWSP inafanya kazi maeneo ya vijijini katika Wilaya 86 kwenye Mikoa 17 ya Tanzania Bara. 

Kwa sasa, Uhakiki wa Program ya Malipo kwa Matokeo (PforR) unaendelea kwa kipindi cha miezi miwili kuanzia tarehe 27 Julai hadi 27 Septemba, 2021