Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

WAKALA WA MAJI NA USAFI WA MAZINGIRA VIJIJINI

"Maji Bombani"

Majukumu ya RUWASA

Majukumu ya RUWASA yametajwa na kufafanuliwa katika kifungu cha 43 cha Sheria ya Huduma za Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira Na. 5 ya mwaka 2019. Kwa ujumla,  RUWASA ina wajibu wa kuendeleza miundombinu kwa kufanya ujenzi na usimamizi wa ujenzi wa miradi ya maji na pia kusimamia utoaji wa huduma endelevu za maji na usafi wa mazingira vijijini. Katika kutekeleza jukumu hilo, RUWASA inafanya shughuli zifuatazo:-

a)

Kuandaa mipango, kusanifu miradi ya maji, kujenga na kusimamia uendeshaji wake

b)

Kuendeleza vyanzo vya maji kwa kufanya utafiti wa maji chini ya ardhi na kuchimba visima pamoja na kujenga mabwawa

c)

Kufanya matengenezo makubwa ya miundombinu ya maji vijijini

d)

Kusajili, kuratibu, kudhibiti, kufuatilia na kutathmini vyombo vya kijamii vinavyohusika na uendeshaji wa huduma ya maji vijijini (Community Based Water Supply and Sanitation Organization - CBWSOs) ili kuhakikisha kuwa huduma inakuwa endelevu.

e)

Kuzijengea uwezo CBWSOs kwa kutoa mafunzo na utaalamu wa uendeshaji na matengenezo ya miradi ya maji vijijini

f)

Kuhamasisha jamii na kutoa elimu ya usafi wa mazingira katika ngazi ya kaya na mtu binafsi (sanitation and hygiene) na masuala ya uhifadhi na utunzaji wa vyanzo vya maji

g)

Kutafuta fedha kwa ajili ya uendeshaji ili kuwezesha RUWASA kutekeleza majukumu yake na kushirikiana na wadau mbalimbali katika masuala yanayohusu utoaji wa huduma za maji na usafi wa mazingira vijijini