Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

WAKALA WA MAJI NA USAFI WA MAZINGIRA VIJIJINI

"Maji Bombani"

Mwenyekiti wa Bodi RUWASA afanya ziara Mkoa wa Geita

Mwenyekiti wa Bodi RUWASA afanya ziara Mkoa wa Geita

Mwenyekiti wa bodi RUWASA afanya ziara Mkoa wa Geita

 

Mwenyekiti wa Bodi ya RUWASA Eng. Ruth Koya amefanya ziara na kukagua mradi wa maji katika kata ya Nkome na Katoma wilaya ya Geita Mkoani Geita unaotekelezawa Na Wakala wa Maji Na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA).

 

Akitoa taarifa ya utekelezi wa mradi huo Meneja wa RUWASA Wilaya ya Geita Mhandisi Sande Batakanwa amesema mradi huo unatekelezwa katika kata 5, za Nkome, Katoma, Nyamboge, Nzera Na Lwezera na utakapokamilika utahudumia wananchi zaidi ya laki moja (100,000) na awamu ya kwanza unatekelezwa katika kata ya Nkome na Katoma zenye wakazi zaidi ya 55,000. Mradi huo unatekelezwa kwa force account na mpaka kukamilka utagarimu zaidi ya bilioni 4.6 ikihusisha Ujenzi wa jengo la pampu, nyumba ya mwendesha mradi, kichoteo cha maji, Ujenzi wa matangi manne (4) yenye ujazo wa Lita 225,000 kwenye mnara wa mita 6, ufungaji wa umeme, Ujenzi mtambo wa kusafishia maji, ununuzi ya pampu 2, ujenzi wa vituo vya kuchotea maji 35, viosiki 3 ulazaji wa bomba kilomita 49. pamoja na Ujenzi wa Nyumba ya CBWSO.

 

Mwenyekiti wa Bodi ya RUWASA Eng. Ruth Koya amewapongeza RUWASA Wilaya na Mkoa wa Geita kwa Namna ambavyo wanatekeleza vyema miradi ya Mji kwa kuzingatia ubora unaohitajika katika kufikia adhima ya serikali ya ‘kumtua mama ndoo kichwani’.

  

Chairperson of the Board of RUWASA Eng. Ruth Koya makes a visit and inspects the water project in the Nkome and Katoma ward of Geita District in Geita Region which is implemented by the Rural Water Supply and Sanitation Agency (RUWASA). Giving information on the implementation of the project, the Manager of RUWASA, Geita District, Engineer Sande Batakanwa said that the project is being implemented in 5 wards, Nkome, Katoma, Nyamboge, Nzera and Lwezera and when it is completed it will serve more than one hundred thousand (100,000) citizens and the first phase is being implemented in Nkome and Katoma county with more than 55,000 inhabitants.

 

The project is being implemented by force account and to completion will cost more than 4.6 billion to complete, involving the construction of a pump building, the project operator's house, a water boiler, the construction of 4 tanks with a capacity of 225,000 liters on a 6 meter raiser, electrical installation, construction water purification plant, purchase of 2 Pumps, construction of 35 water extraction stations, 3 viosiki, pipe laying 49 km. as well as construction of CBWSO House.

 

Chairperson of the Board of RUWASA Eng. Ruth Koya has congratulated RUWASA District and Geita Region for the manner in which they are successfully implementing the City's projects in accordance with the quality required to achieve the Government's mission of ‘Kumtua Mama Ndoo Kichwani’.