Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

WAKALA WA MAJI NA USAFI WA MAZINGIRA VIJIJINI

"Maji Bombani"

Waziri wa Maji Mhe. Aweso - Aanza ziara Mkoa wa Lindi

Waziri wa Maji Mhe. Aweso - Aanza ziara Mkoa wa Lindi

AWESO AANZA ZIARA LINDI KWA KUTEKELEZA MAELEKEZO YA WAZIRI MKUU; AGAWA PIKIPIKI KWA CBWSOs

Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso anaeendelea na ziara ya kikazi mkoani Lindi katika kukagua na kusimamia utekelezaji wa Miradi ya Maji ambapo ameanza kwa kutekeleza maagizo ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa aliyoifanya tarehe 08 Januari, 2024 Mkoani humo. Waziri Aweso alianza kazi hiyo kwa kugawa pikipiki kwa Vyombo vya Utoaji  huduma ya Maji Ngazi ya Jamii (CBWSOs).

Akiwa na viongozi wa Mkoa wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe Zainab Telack amegawa jumla ya Pikipiki 22 kwa CBWSO 19 kwa ajili ya usimamizi na uendeshaji wa skimu za Maji vijijini.  Lengo kuu la kugawa pikipiki hizo ni kurahisisha utendaji kazi wa CBWSO’s kutokana na ukubwa wa maeneo ya kutolea huduma.