Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

WAKALA WA MAJI NA USAFI WA MAZINGIRA VIJIJINI

"Maji Bombani"

Mwenyekiti wa Bodi  Atembelea Mradi Mkubwa wa Maji -  Ruangwa

Mwenyekiti wa Bodi Atembelea Mradi Mkubwa wa Maji - Ruangwa

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi RUWASA Mhandisi Ruth Koya ametembelea mradi mkubwa wa maji unaotekelezwa na RUWASA katika vijiji 56 vya Wilaya za Ruangwa, Nachingwea na Lindi vijijini. 

Mhandisi Koya ameridhishwa na utekelezaji wa mradi kwa kipande cha pili kinachotekelezwa na kampuni ya Emirates Builders Co.Ltd. Akiwa eneo la Ujenzi wa tangi la ujazo wa lita milioni tatu (lita milioni 3), Mhandisi  Koya aliipongeza RUWASA kwa usimamizi mzuri wa utekelezaji wa mradi na kusisitiza kuongeza kasi ili mradi ukamilike kwa wakati.

Mkandarasi ana jukumu la kujenga matangi matano, chanzo cha maji, nyumba za watumishi, ofisi, vituo viwili vya kusukuma maji na kulaza bomba urefu wa kilomita mia mbili.