Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

WAKALA WA MAJI NA USAFI WA MAZINGIRA VIJIJINI

"Maji Bombani"

Utekelezaji wa Miradi Mwaka wa Fedha 2023/2024

Katika mwaka wa fedha 2023/2024, Wakala ulipanga kutekeleza jumla ya Miradi 1,546 katika mikoa 25 nchini, inayogharimu kiasi cha Tshs 500,342,398,033.25. Miradi hiyo inategemewa kuhudumia watu wapatao 2,274,193 katika vijiji 844.

Katika kipindi cha nusu mwaka wa fedha 2023/2024, hadi kufikia Desemba 31, 2023 jumla ya miradi 374 iliyogharimu kiasi cha Tshs 128,177,655,882 ilikuwa imekamilika. RUWASA inaendelea na utekelezaji wa miradi 1,172 iliyobakia ili kutimiza  adhma ya serikali ya kutoa huduma ya uhakika ya Maji Safi na Salama vijijini.