Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

WAKALA WA MAJI NA USAFI WA MAZINGIRA VIJIJINI

"Maji Bombani"

Mwenyekiti wa Bodi RUWASA afanya ziara Mkoani Iringa

Mwenyekiti wa Bodi RUWASA afanya ziara Mkoani Iringa

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi - RUWASA Mhandisi Ruth Koya pamoja na baadhi ya wajumbe wa Bodi hiyo wameanza ziara ya kutembelea na kukaguzi miradi na skimu za maji vijijini.

 Ziara hiyo imeanza leo Mkoani Iringa Wilaya ya Iringa vijijini ambapo walitembelea mradi wa upanuzi wa Skimu ya Izazi kwenda kijiji cha Mkumbwanyi.

 Akiwa kwenye mradi Mhandisi Koya amewapongeza RUWASA na wananchi wa maeneo hayo na kuwataka watunze mradi ili uendelee kuwanufaisha.


 Kwa upande wao wananchi wa vijiji hivyo wameishukuru Serikali kwa kuwasogezea huduma ya maji karibu na maeneo yao.