Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

WAKALA WA MAJI NA USAFI WA MAZINGIRA VIJIJINI

"Maji Bombani"

Waziri wa Maji akikagua Tangi la maji  katika mradi wa maji wa Dabalo  - Chamwino

Waziri wa Maji akikagua Tangi la maji katika mradi wa maji wa Dabalo - Chamwino

Waziri wa Maji akikagua tangi la Plastiki liloyotumiwa katika ujenzi wa mradi wa maji wa Dabalo  Wilaya ya Chamwino  Mkoa wa Dodoma, ambapo ameipongeza RUWASA kwa kushirikiana na PLASCO katika kufanikisha utengenezaji na matumizi ya tangi hilo lenye ujazo wa lita 150,000 limewekwa katika chanzo cha maji na yanadumu kwa muda wa zaidi ya miaka 60.


Hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi imefanyika Julai 15, 2022 katika Kata ya Dabalo ulipo mradi huo unaogharimu zaidi ya Shilingi Milioni 907. Mradi unatekeelzwa na RUWASA chini ya Meneja wa Mkoa na Wilaya ya Chamwino kwa fedha za Mfuko wa Maji wa Taifa. Mradi unajengwa na Mkandarasi Medes Company Limited na unatarajiwa kuhudumia wakazi 8,134 ambapo unatarajiwa kukamilika mapema kabla ya Julai 20 2022.