Mafunzo ya kuomba msamaha wa VAT kwa kutumia Mfumo yakiendelea Mikoa ya Kanda ya Kusini ambapo Mameneja wa RUWASA wa Mikoa, Wilaya na Maafisa wa Mikoa ya Mbeya, Songwe, Iringa, Njombe na Rukwa wameshiriki. Mafunzo yanaendeshwa na timu ya wataalamu kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Makao Makuu Kuanzia tarehe 24 - 25 Januari, 2022.
Baada ya kukamilika kwa mafunzo hayo kwa kanda zote, Maombi ya Msamaha wa Kodi ya Ongezeko la Thamani yatakuwa yanafanyika kupitia Mfumo.