Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

WAKALA WA MAJI NA USAFI WA MAZINGIRA VIJIJINI

"Maji Bombani"

Waziri wa Maji aipongeza RUWASA

Waziri wa Maji aipongeza RUWASA

Waziri wa Maji  Mhe. Jumaa Aweso ameipongeza RUWASA kwa kuwa na mikakati madhubuti ya ukamilishaji wa Miradi ya Maji pamoja na kuhakikisha inakuwa endelevu. Waziri ameyasema hayo wakati wa kikao kati ya Menejimenti ya RUWASA na Menejimenti ya Wizara ya Maji ambapo RUWASA iliwasilisha taarifa ya utekelezaji. Mhe. Waziri wa Maji ameridhishwa na kasi ya RUWASA ya kutekeleza miradi ya maji 115 kati 177 iliyokuwa imekamilika lakini ikawa haitowi maji wakati RUWASA inaanzishwa. Aidha, Mhe. Waziri ametoa maelekezo kwa menejimenti ya RUWASA kuhakikisha kuwa miradi ya maji 62 iliyosalia inakamilika kwa wakati.