Rais mstaafu wa awamu ya nne Mhe. Jakaya Kikwete amesema RUWASA inawafanya kazi nzuri ya kuwapatia wananchi waishio maneno ya vijijini majisafi na salama.
Msataafu Kikwete alitoa pongezi na sifa hizo leo Oktoba 6, 2022 alipotembelea banda la Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) lililopo kwenye maonesho ya Wiki ya Uwekezaji na Biashara Mkoa wa Pwani. Maonesho yanafanyika kwenye viwanja vya steni ya zamani ya Kibaha Mailimoja Mkoa wa Pwani.
''Ninyi RUWASA ni watu wazuri sana'' alisema Rais Mstaafu Jakaya Kikwete bada ya kupata maelezo ya utekelelezaji wa miradi ya maji na mikakati ya Wakala kutoka kwa Meneja wa kitengo cha Uhusiano na Masoko wa RUWASA Makao Makuu (Bw. Athumani Shariff)
Katika maonesho hayo yanayofanyika kwa siku tano kuanzia Oktoba 5, 2022 RUWASA inatoa elimu kuhusu utekezaji wa miradi ya maji pamoja na mwelekeo wa Taasisi ikiwa ni pamoja na ujio wa teknolojia ya kutumia dira a maji za malipo ya kabla ya matumizi (Pre paid water meters) zinazofanyiwa majaribio katika maeneo mbalimbali nchini ikiwa ni hatua ya kuboresha huduma na kuondoa changamoto kwenye miradi ya maji hususani maeneo ya vijijini.