Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) ameshuhudia zoezi la utiaji saini mikataba ya mradi wa kubuni, kutengeneza na kufunga Dira za Maji za malipo kabla ya matumizi kati ya RUWASA na Chuo cha Ufundi Arusha (ATC), Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) na DTBi (Dar Teknohama and Business Incubator) wanaoshirikiana na Chuo cha Uhandisi na Ufundi cha Al Maktoum.
Katika awamu ya kwanza taasisi hizo zitatengeneza na kufunga dira 300, baadae mradi huo utapelekwa kwenye maeneo mengi zaidi kulingana na uhitaji.