Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

WAKALA WA MAJI NA USAFI WA MAZINGIRA VIJIJINI

"Maji Bombani"

RUWASA yawapa elimu wahariri wa vyombo vya habari kuhusu masula ya maji

RUWASA yawapa elimu wahariri wa vyombo vya habari kuhusu masula ya maji

Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) imekutana na Wahariri wa Vyombo mbalimbali vya Habari vya hapa nchini kwa lengo la kuwapa semina ya uelewa juu ya taasisi hiyo yenye jukumu la kujenga na kusimamia miradi ya maji Vijijini ikiwa ni kundi muhimu katika kuhabarisha na kuelimisha umma kupitia vyombo vyao.

Semina hiyo iliyoongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Wakala huyo Mhandisi Clement KIVEGALO, sambamba na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Bwai Biseko, Mkurugenzi wa Usambazaji Maji Mhandisi Mkama Bwire, Mwanasheria Gloria Chegeni na Meneja Uhusiano na Masoko Athuman Shariff, ilifanyika katika Ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam Novemba 1, 2022.