Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

WAKALA WA MAJI NA USAFI WA MAZINGIRA VIJIJINI

"Maji Bombani"

RUWASA yaleta ubunifu wa Dira za  malipo ya Kabla

RUWASA yaleta ubunifu wa Dira za malipo ya Kabla

Mhe. Selemani Jafo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira (Kulia) akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Masoko wa Wakala wa Maji na Usafi wa mazingira Vijijini Bwana Athuman Shariff (Kushoto) namna Dira za Maji za Malipo ya kabla ya matumizi (Prepaid Water Meter) inavyofanyakazi.

Ubunifu huo ulifanyika wakati Waziri Jafo alipokuwa akikagua mabanda ya maonesho ya Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maji. Maonesho yalifanyika katika Hotel ya Hyatt Refence The Kilimanjaro Jijini Dar es Salaam Agosti 19, 2022.

Maonesho hayo yameenda sambamba na Mkutano wa Mawaziri wa Maji wa Nchi 11 zinazotumia chanzo cha maji cha Bonde la Mto Nile. Katika maoesho hayo, Waziri Jafo alikuwa mgeni rasmi akimwakilisha Mhe. Dkt. Phillip Mpango, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania.