Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

WAKALA WA MAJI NA USAFI WA MAZINGIRA VIJIJINI

"Maji Bombani"

Baraza la Wafanyakazi  RUWASA Lazinduliwa

Baraza la Wafanyakazi RUWASA Lazinduliwa

Mgeni rasmi Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) amehudhuria katika hafla ya uzinduzi wa Baraza la Wafanyakazi la Wakala wa maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) tarehe 29 Agosti, 2022 Jijini Dodoma katika Ukumbi wa Jenerali Mabeyo.

Katika hafla hiyo, Mgeni rasmi Mhe. Jumaa Aweso aliwapongeza RUWASA kwa kuunda Baraza la Wafanyakazi kwa sababau ni takwa halalili la Kisheria. Mgeni rasmi alisisitiza kuwa, wafanyakazi wote walitumie vizuri baraza hilo kwa ustawi wa wafanyakazi na Taasisi ili pande zote mbili zinufaike na zifikie malingo ya msingi yaliyopangwa kutekelezwa.

Awali kabla ya kumkaribisha mgeni Rasmi, Kaimu Mkurugenzi  Mkuu wa RUWASA Bwai Biseko alisema, kuundwa kwa Baraza la Wafanyakazi  ni takwa la kisheria hivyo taasisi hiyo imeunda Baraza hilo ili kutoa fursa kwa wafanyakazi kujadili mambo mbalimbali yanayowahusu na kuishauri taasisi katika kuboresha tija mahala pa kazi na kuzingatia  haki na wajibu wa pande zote mbili.