Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

WAKALA WA MAJI NA USAFI WA MAZINGIRA VIJIJINI

"Maji Bombani"

Watumishi RUWASA wapigwa msasa e-OFFICE

Watumishi RUWASA wapigwa msasa e-OFFICE

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa RUWASA Bwai Biseko amewaasa watumishi wa taasisi hiyo kuzingatia matumizi sahihi ya taarifa zinazoingia na kutoka ili kupata matokeo chanya ikiwemo kuwezesha viongozi kufanya maamuzi sahihi na kwa wakati. Biseko ametoa wito huo wakati akifungua mafunzo ya utunzaji wa kumbukumbu na matumizi ya mfumo wa taarifa unaofahamika kama e-Office leo Julai 12, 2023 yanayofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma.

 Alisema kwamba taarifa na kumbukumbu ni nyenzo muhimu katika utendaji kazi wa taasisi ili kufikia malengo. Matumizi mabaya ya taarifa za taasisi zina athari mbaya ikiwemo mtumishi kutoa taarifa za uongo au kupotosha jambo ambalo linaweza kumtia matatani ikiwemo kushtakiwa kwa jinai na hata uhujumu uchumi. 


Mafunzo hayo yatafanyika kwa siku mbili na yanaendeshwa na Maafisa kutoka Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa.