Waziri wa Maji Mhe.
Jumaa Aweso amezindua Bodi mpya ya Wakurugenzi ya Wakala wa Maji na Usafi wa
Mazingira Vijijini (RUWASA) katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa PSSSF
jijini Dodoma Juni 27, 2023.
Bodi hiyo chini ya Mwenyekiti
wake Mhandisi Ruth Koya itahudumu kwa miaka mitatu ambapo katika hotuba yake
Mhe. Waziri Aweso alisema ana imani kubwa na bodi hiyo kutokana na uzoefu wa
wajumbe wake katika sekta yam aji kwa ujumla.
Waziri Aweso pia
‘aliimwagia’ sifa Bodi ya Kwanza ya RUWASA iliyomaliza muda wake chini ya
Mwenyekiti wake Prof. Idrissa Mshoro ambayo imehudumu kwa kipindi cha miaka
mitatu baada ya kuanzishwa kwa RUWASA, kwa kazi kubwa ya kuiongoza na
kuisimamia taasisi katika majukumu ya kusanifu, kujenga, na kutoa huduma ya
majisafi kwa wananchi waishio vijijini.