Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

WAKALA WA MAJI NA USAFI WA MAZINGIRA VIJIJINI

"Maji Bombani"

CPA Msiru awataka wananchi kuchangia huduma ya maji

CPA Msiru awataka wananchi kuchangia huduma ya maji

Mkurugenzi wa usambazaji maji safi na usafi wa mazingira kutoka Wizara ya Maji CPA. Joyce Msiru amewaasa wananchi wa Kimala Wilayani Kilolo Iringa kutunza miundombinu ya miradi ya maji na kuepuka uharibifu wa mazingira na kuhakikisha wanatunza vyanzo vya maji ili miradi inayojengwa iweze kudumu nakutoa huduma endelevu. Msiru aliyasema hayo katika kijiji cha Kimala wilaya ya Kilolo mkoani Iringa, alipoungana na timu ya wataalamu wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijini (Ruwasa).

Kwa upande wao wananchi wa Kimala wakizungumza kwa nyakati tofauti wamesema, tatizo la maji katika kijiji cha Kimala kilichopo mpakani mwa Mikoa ya Iringa na Morogoro ni la miaka mingi na lime sababisha wakazi wa kijiji hicho kutumia muda mwingi kutafuta maji kwa matumizi ya kila siku badala ya kufanya kazi nyingine za uzalishaji mali.

RUWASA inaendelea kuwekeza fedha na kujenga miradi ya maji ili huduma hiyo iweze kuwafikia wananchi wengi katika vijiji mbalimbali hapa nchini. Mradi wa maji wa Kimala umeshaanza kutoa huduma ya maji ingawa bado upo asilimia 75 ya utekelezaji. Utakapokamilika utagharimu Shilingi 561,490,794.38. Mkurugenzi Mkuu wa RUWASA Mhandisi KIVEGALO amesema ni wajibu wa wakala wa maji kumaliza tatizo la maji kwa wananchi na imejipanga kufikia lengo hilo kwa kutekeleza miradi ya maji kwenye meneo yasiyokuwa na huduma hiyo.

KIVEGALO amewataka wananchi wa kijiji hicho na vingine ambavyo RUWASA inatekeleza ujenzi wa miradi ya maji kuchangia gharama za maji ili huduma hiyo iwe endelevu badala ya kurudi walikotoka kutumia vyanzo visivyo rasmi.