Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

WAKALA WA MAJI NA USAFI WA MAZINGIRA VIJIJINI

"Maji Bombani"

Miradi ya Maji 1,029 kutekelezwa Mwaka wa Fedha 2022 -2023

Miradi ya Maji 1,029 kutekelezwa Mwaka wa Fedha 2022 -2023

Miradi ya Maji 1,029 kutekelezwa Mwaka wa Fedha 2022 -2023ambapo kati ya hiyo, miradi 381 ni mipya na miradi 648 ni ile inayoendelea kutekelezwa ambapo zaidi ya Shilingi bilioni 387.7  zimeidhinishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ajili ya utekelezaji wa miradi hiyo.  Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu Mhandisi Clement KIVEGALO katika Ukumbi wa Habari MAELEZO Jijini Dodoma.

Mhandisi KIVEGALO aliyasema hayo katika mkutano na waandishi wa Habari leo Jijini Dodoma katika ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO uliopo katika jengo la PSSSF House Makole Jijini Dodoma, ambapo Mkurugenzi huyo amesema kwa Mwaka huu wa fedha ailimia ya upatikanaji wa maji vijijini zinatarajiwa kupanda kwa asilimia sita kutoka asilimia 74.5 ya sasa hadi kufikia asilimia 80.5