Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

WAKALA WA MAJI NA USAFI WA MAZINGIRA VIJIJINI

"Maji Bombani"

Timu ya Ununuzi RUWASA yapata mafunzo ya TANePS

Timu ya Ununuzi RUWASA yapata mafunzo ya TANePS

Wajumbe wa RUWASA wa Bodi ya Ununuzi, Bodi Ndogo ya Zabuni na Maafisa wa Ununuzi wamekamilisha mafunzo ya  TANePS Mkoani Singida. Mafunzo haya yamefanyika kwa muda wa siku tano yakiwa na lengo la kuwajengea uwezo ili kuleta tija na kuhakikisha michakato ya ununuzi kuanzia ngazi za Mikoa na wajumbe wa bodi za Ununuzi. Mafunzo yamefungwa na Mkurugenzi Mkuu wa RUWASA Mhandisi Clement KIVEGALO kwa kuwasihi wajumbe wote walioshiriki mafunzo hayo kutumia ujuzi na weledi walioupata ili kuhakikisha kuwa mchango wao kwenye Taasisi unakuwa na tija kwa kuwa eneo la ununuzi limebeba sehemu kubwa ya utekelezaji wa miradi ya maji.

Tanzania Census 2022