Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

WAKALA WA MAJI NA USAFI WA MAZINGIRA VIJIJINI

"Maji Bombani"

Rais Ahitimisha Kilele cha Wiki ya Maji

Rais Ahitimisha Kilele cha Wiki ya Maji

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema kuwa, mabadiliko ya kimfumo yaliyopelekea kuundwa kwa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini - RUWASA, yamesaidia kuboresha usimamizi wa miradi ya maji nchini na kuongeza kasi ya utekelezaji wake. Rais Samia aliyasema hayo wakati wa siku ya maji duniani Machi 22 katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. 

Rais Samia amesema RUWASA imeongeza nidhamu ya utendaji kwa wahandisi ambao awali walikuwa chini ya Ofisi ya Rais TAMISEMI. "Mfumo umesaidia kuleta ufanisi na sasa kazi za maji zinakwenda vizuri haswa vijijini. Kwa ujumla Wizara ya Maji inafanya kazi nzuri" alisema Rais Samia.