Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Mhandisi Clement KIVEGALO akisaini mkataba na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni kwa ajili ya Ujenzi wa Bwawa la Kwekambala. Hafla hiyo imefanyika katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Handeni tarehe 27 Julai, 2021.Ujenzi wa Bwawa la Kwekambala utasaidia kuondoa kwa kiasi kikubwa tatizo la upatikanaji wa majisafi na salama kwa wananchi waishio katika Wilaya ya Handeni.