Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

WAKALA WA MAJI NA USAFI WA MAZINGIRA VIJIJINI

"Maji Bombani"

Kitengo cha Huduma za Kisheria

Kitengo hiki hufanya shughuli zifuatazo: -

i)

Kutoa huduma za kisheria na msaada juu ya tafsiri ya sheria, masharti ya mkataba na mikataba ya ununuzi;

ii)

Kutoa msaada wa kiufundi katika kuandaa muswada /sheria inayopendekezwa;

iii)

Kushiriki mazungumzo na mikutano RUWASA yenye kuhitaji utaalam wa sheria;

iv)

Tafsiri sheria ndani ya RUWASA;

v)

Kuwasiliana na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali juu ya kesi za madai na madai mengine yanayohusu RUWASA;

vi)

Kuandaa na kukagua vyombo mawasiliano ya kisheria kama vile maagizo, notisi, vyeti na makubaliano;

vii)

Kuhakiki mikataba kabla ya kusainiwa;

viii)

Kushuhudia na kutia saini  mikataba ya kazi; na

ix)

Kuwakilisha/ kutetea Wakala kwenye mahakama kwenye mambo yote ya kimkataba