Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani kinaongozwa na Mkaguzi Mkuu wa ndani na hufanya
shughuli zifuatazo:
i) |
Kuandaa na kutekeleza Mipango ya kimkakati ya Ukaguzi; |
ii) |
Kupitia na kuripoti juu ya udhibiti mzuri wa upokeaji,
utunzaji na matumizi ya rasilimali zote za kifedha za Wakala; |
iii) |
Kupitia na kuripoti juu ya kufuata taratibu za kifedha na
kiutendaji zilizowekwa katika sheria yoyote au kanuni yoyote au maagizo ya
udhibiti wa matumizi ya Wakala; |
iv) |
Kupitia na kuripoti juu ya uainishaji sahihi wa mapato na
matumizi; |
v) |
Kubuni taratibu za ukaguzi ii kukidhi Viwango vya Kimataifa; |
vi) |
Kupitia na kutoa ripoti juu ya umadhubuti na kuaminika kwa
taarifa za kifedha na uendeshaji pamoja na kuandaa ripoti za kifedha na
nyingine; |
vii) |
Kupitia na kutoa ripoti juu ya mifumo iliyotumika kutunza
mali, na kuthibitisha uwepo wa mali hizo; |
viii) |
Kupitia na kuripoti juu ya shughuli au mipango ili kuhakikisha
matokeo yanaambatana na malengo; |
ix) |
Kupitia na kutoa ripoti juu ya majibu ya uongozi kwenye ripoti
za ukaguzi wa ndani, na pamoja na kufuatilia na kusaidia menejimenti
kusimamia utekelezaji wa mapendekezo yaliyotolewa na ripoti na Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali; |
x) |
Kupitia na kutoa ripoti juu ya Wakala; |
xi) |
Kufanya ukaguzi wa tathmini ya miradi ya maji na usafi wa
mazingira vijijini |