Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

WAKALA WA MAJI NA USAFI WA MAZINGIRA VIJIJINI

"Maji Bombani"

Kitengo cha Uhusiano na Masoko

Kitengo hiki kina majukumu yafuatayo: -

i)

Kuandaa na kutekeleza Sera ya Uhusiano ya Wakala;

ii)

Kuongeza uelewa wa umma kwa jamii za vijijini kwenye sual la  usafi, elimu ya usafi; ulinzi na uhifadhi wa vyanzo vya maji;

iii)

Kukuza ushirikiano baina ya Wakala, mashirika ya ndani na ya kimataifa;

iv)

Kuandaa na kutekeleza mikakati na mipango ya kisoko;

v)

Kuratibu matangazo ya Wakala yenye kuufahamisha umma kuhusu shughuli zake

vi)

Kufanya mpango wa utangazaji wa kukuza muonekano wa RUWASA;

vii)

Kuhakikisha tovuti na akaunti zake kwenye mitanadao ya kijamii inakwenda kwa wakati

viii)

Andaa Mkakati wa Mawasiliano na muundo wake kwa RUWASA;

ix)

Tumia tekinolojia za kimtandao kuboresha muonekano wa RUWASA na upatikanaji wake kwenye mitandao ya kijamii;

x)

Andaa mikutano mbalimbali na vyombo vya habari pamoja na waandishi wa habari kwa ajili ya kuwaspa muhtasari wa taarifa;

xi)

Kukuza ushiriki wa jamii na kuelimisha umma kuhusu huduma ya maji na usafi wa mazingira kwa kushirikiana na wadau mbalimbali;

xii)

Kuratibu utayarishaji, utengenezaji na usambazaji wa vipeperushi, nakala na majarida kwa Umma;

xiii)

Kufanya tafiti za soko;

xiv

Tathmini shughuli za uuzaji na kupendekeza maboresho;

xv)

Kuandaa vifaa vya mawasiliano ili kukuza biashara ya RUWASA

xvi)

Kuratibu Mikutano ya Waandishi wa Habari