Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

WAKALA WA MAJI NA USAFI WA MAZINGIRA VIJIJINI

"Maji Bombani"

Mpango wa Malipo kwa Matokeo (PbR)

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na Idara ya Maendeleo ya Kimataifa (DFID) ya nchini Uingereza (UK) - inatekeleza mpango wa malipo wenye kuzingatia matokeo (PBR) katika kusaidia awamu ya pili ya Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji maeneo ya vijijini.

Lengo kuu ni kuchochea maendeleo katika kuboresha ufanisi wa huduma za maji kwa kutoa motisha kwa RUWASA (kupitia vigezo vilivyowekwa) ili iweze kukarabati, kupanua miradi na kuhamasisha jamii kushiriki kikamilifu katika uendelevu wa miradi hiyo. Mpango huu unaotekelezwa kwenye mikoa yote 26 ya Tanzania Bara na wenye kudhaminiwa na Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji (WSDP-II) ulianza Mwezi Juni, 2012 na unatarajiwa kuisha Mwezi Machi, 2022. 

Mpango huu umekuwa uitekelezwa kwa awamu kuanzia awamu ya kwanza na sasa upi awamu ya sita. kwa sasa uhakiki wa awamu ya sita unatarajia kuanzia  tarehe 5 Septemba hadi 3 Octoba, 2021