Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

WAKALA WA MAJI NA USAFI WA MAZINGIRA VIJIJINI

"Maji Bombani"

Programu ya Malipo kwa Matokeo (PforR)

Programu ya Malipo kwa Matokeo (PforR) ni mpango ulianzishwa na Benki ya Dunia (Word Bank) na ulianza Julai 15, 2019 ikiwa ni sehemu ya program ya uhakika wa usalama wa maji na usafi wa mazingira  vijijini (sub-program under the Sustainable Rural Water Supply and Sanitation Program – (SRWSP)).

Malengo ya Programu ya Malipo kwa Matokeo (PforR) ni kuchochea kasi ya utekelezaji wa Mpango wa Uboreshaji Huduma ya Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini kupitia motisha zilizowekwa kwa viashiria ambavyo hupimwa kupitia mafanikio ya utekelezaji wa kazi mbalimbali kwenye wilaya 86 na mikoa 17 Tanzania Bara.

Matokeo ya Program ya Malipo kwa Matokeo

Program ya Malipo kwa Matokeo (PforR) imesaidi wananchi wa Wilaya ya Kishapu Mkoa wa Shinyanga kupata Huduma ya maji safi na salama

Mwezi Machi, 2023, Mikoa nane (8) ilijumuishwa kwenye utekelezaji wa Program ya Malipo kwa Matokeo ambapo hapo awali haikuwa sehemu ya program. Mikoa hiyo ni Arusha, Kilimanjaro, Tanga, Pwani, Morogoro, Njombe, Mbeya na Dodoma. Kwa sasa, program inatekelezwa kwenye Mikoa 25 na Wilaya 137.

Matokeo ya tathmin ya program ya PforR iliyofanyika awamu ya tatu kuanzia Julai hadi Septemba 2022 imeonesha matokeo chanya ambapo RUWASA imefanikisha upatikanaji wa zaidi ya shilingi bilioni 377.24 ukilinganisha na awamu ya pili  ambapo matokeo yaliwezesha upatikanaji wa wastani wa shilingi  bilioni 250.

Pamoja na mafanikio hayo yaliyofikiwa wakati wa utekelezaji wa progamu, Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Maji imedhamiria kuwasilisha pendekezo la ongezeko la fedha kutoka benki ya dunia kutokana na mafanikio sambamba na muelekeo wa sekta ya maji na kukabiliana na changamoto zinazoikabili ya sekta ya maji kwa sasa.

Pamoja na hayo, Benki ya Dunia kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania wameandaa ripoti ya mazingira itakayotumika kama mwongozo wakati wa uandaaji wa miradi ya maji na usafi wa mazingira vijijini pamoja na kutoa tathmin ya kuelekea uongezwaji wa fedha za miradi. Ripoti hiyo imewekwa wazi kwa wadau kutoa maoni yao. 

Kwa maelezo zaidi, bonyeza hapa chini kupata taarifa zaidi.

 Taarifa ya Tathmini ya Mifumo ya Mazingira na Kijamii (ESSA) - Additional Financing PforR