Kutokana na Sheria ya Usambazaji Maji na Usafi
wa Mazingira Namba 5 ya 2019, RUWASA imepewa jukumu la kuhakikisha jamii za
wananchi waishio maeneo ya vijijini ndani ya Tanzania Bara zinapata huduma ya
maji safi na salama. Aidha, RUWASA inawajibika kutoa huduma za maji katika
maeneo maalumu ya mijini kwa maelekezo ya Waziri mwenye dhamana ya sekta ya
maji.
Huduma za maji katika maeneo ya vijijini
husimamiwa na kuendeshwa na Vyombo vya Usimamizi wa Huduma za Maji Ngazi ya
Jamii (CBWSOs) chini ya usimamizi wa RUWASA katika ngazi ya Wilaya. Ili kuhakikisha
uendelevu wa huduma za usambazaji maji, CBWSO hukusanya tozo za maji kutoka kwa
jamii kama ilivyojadiliwa na kukubaliwa katika vyombo husika.
Aidha, CBWSO inawajibika katika kufanya
matengenezo ya mradi ili kuhakikisha jamii inapata huduma ya maji safi na
salama kila siku.