Majukumu
ya RUWASA yametajwa na kufafanuliwa katika kifungu cha 43 cha Sheria ya Huduma
za Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira Na. 5 ya mwaka 2019. Kwa ujumla,
RUWASA ina wajibu wa kuendeleza miundombinu kwa kufanya ujenzi na usimamizi wa
ujenzi wa miradi ya maji na pia kusimamia utoaji wa huduma endelevu za maji na
usafi wa mazingira vijijini. Katika kutekeleza jukumu hilo, RUWASA inafanya
shughuli zifuatazo:-
a) |
Kuandaa
mipango, kusanifu miradi ya maji, kujenga na kusimamia uandeshaji wake |
b) |
Kuendeleza
vyanzo vya maji kwakufanya utafiti wa maji chini ya ardhi nakuchimba visima
pamoja na kujenga mabwawa |
c) |
Kufanya
matengenezo makubwa ya miundombinu ya maji vijijini |
d) |
Kusajili,
kuratibu, kudhibiti, kufuatilia na kutathmini vyombo vya kijamii
vinavyohusika na uendeshaji wa huduma ya maji vijijini (Community Based Water
Supply and Sanitation Organization - CBWSOs) ili kuhakikisha kuwa huduma
inakuwa endelevu. |
e) |
Kuzijengea
uwezo CBWSOs kwa kutoa mafunzo na utaalamu wa uendeshaji na matengenezo ya
miradi ya maji vijijini |
f) |
Kuhamasisha
jamii na kutoa elimu ya usafi wa mazingira katika ngazi ya kaya na mtu
binafsi (sanitation and hygiene) na masuala ya uhifadhi na utunzaji wa vyanzo
vya maji |
g) |
Kutafuta
fedha kwa ajili ya uendeshaji ili kuwezesha RUWASA kutekeleza majukumu yake
na kushirikiana na wadau mbalimbali katika masuala yanayohusu utoaji wa
huduma za maji na usafi wa mazingira vijijini |