RUWASA ililithi jumla ya skimu 1,379 za maji kutoka TAMISEMI. Kati ya hizo, skimu 177 zilikuwa na changamoto za utoaji wa huduma ya maji kwa wa wananchi, skimu 1,202 zilikuwa zimekamilika.
Kwa mwaka wa fedha 2021/2022 RUWASA imepanga kujenga jumla ya miradi ya maji 1,527
Kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022, RUWASA imejenga na kukamilisha jumla ya miradi ya maji 1,176
Mikakati ya RUWASA kuhusu mapinduzi ya utoaji wa huduma ya maji hususani maeneo ya vijijini ni pamoja na:-
1. Ujenzi wa miradi ya maji yenye ubora na kujali thamani ya fedha.
2. Utoaji wa huduma ya maji kwa kutumia mita za malipo ya kabla ya matumizi (Prepaid Water Metres)