Chombo cha Watoa Huduma ya Maji Ngazi ya Jamii (CBWSOs) ni chombo cha kijamii kilichoundwa na kusajiliwa kisheria kwa ajili ya kuendesha na kusimamia miradi wa maji ili iweze kutoa huduma ya maji endelevu kwa wananchi waishio maeneo ya vijijini.
Chombo cha Watoa Huduma ya Maji Ngazi ya Jamii (CBWSO) kinasajiliwa na Meneja wa RUWASA ngazi ya Wilaya baada ya Jumuiya hiyo kukidhi vigezo ya usajili. Vigezo vya Usajili vinapatika kwenye Sheria na Mwongozo wa Vyombo.
Meneja wa RUWASA Wilaya anaweza kufuta usajili wa CBWSO endapo ataona haridhishwi na mwenendo wa uendeshaji wa mradi husika rejea kanuni No.829/05/11/2019, 21(1)
Bei za maji zinapendekezwa na Chombo husika kinachosimamia mradi kulingana na mwongozo wa upangaji bei za maji ulioandaliwa na RUWASA. Aidha, tozo ya maji huidhinishwa na Bodi ya RUWASA