Ndiyo, RUWASA kupitia Sehemu ya Uchimbaji inachimba visima maeneo mbalimbali nchini.
Gharama za kuchimba kisima/Visima hutegemea zaidi mambo yafuatayo:-
1. Kipenyo na kina cha kisima pamoja na bomba zitakazotumika katika ujenzi.
2. Aina ya mwamba ulionekana wakati wa utafiti wa maji chini ya ardhi.
3. Umbali wa eneo la kuchimba kisima kutoka mahali ilipo mitambo ya uchimbaji.
4. Bei ya vifaa na mafuta (Dizeli) kwa wakati husika.
5. Vifaa vitakavyotakiwa kupelekwa eneo la uchimbaji kwa ajili ya shughuli, hiyo mfano booster, compresor, mudpump, generator, welding plant, mobile workshop.
6. Muda utakaotumika kupima uwezo wa utoaji maji wa kisima husika.
7. Kiasi na gharama za gravel, polymer bentonite, diesel, lubricants nk. vitakavyotumika katika uchimbaji.
Aidha, wastani wa gharama za uchimbaji zinatofautiana kulingana na miamba ya eneo husika kwa mfano: Miamba laini gharama ni kati ya shilingi (80,000 hadi 100,000) kwa mita moja, miamba migumu gharama ni kati ya shilingi (100,000 hadi 120,000) kwa mita moja na maeneo ya kwenye mawe gharama ni shilingi (120,000 hadi 150,000) kwa mita moja.
Ukitaka kuchimba kisima unatakiwa kufanya utafiti wa awali ili:-
Gharama za ujenzi wa bwawa zinategemea mambo yafuatayo:-
Faida za kufanya utafiti kabla ya kuchimba kisima/ kujenga bwawa ni kama ifuatavyo:-