Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

WAKALA WA MAJI NA USAFI WA MAZINGIRA VIJIJINI

"Maji Bombani"

Mitambo yaendeleza kasi ya uchimbaji visima maeneo ya vijijini

Mitambo 25 ya kuchimba visima virefu iliyokabidhiwa kwa RUWASA mwishoni mwa mwaka 2022 tayari ipo katika maeneo mbalimbali ya nchini ikiendelea na kazi ya uchimbaji wa visima hususani maeneo ya vijijini.  Hadi kufikia mwezi Machi, 2023, mitambo hiyo ilikuwa imeshachimba jumla ya visima 88 katika maeneo mbalimbali nchini.