RUWASA kwa kushirikiana na Wizara ya Afya,
Wizara ya Elimu na OR-TAMISEMI kwa pamoja zina jukumu la kuhakikisha huduma za
usafi wa mazingira zinazingatiwa na kutekelezwa katika maeneo ya vijijini. Hata
hivyo, RUWASA inapaswa kuchochea na kuhamasisha jamii za vijijini kuzingatia
usafi wa mazingira pamoja na kulinda na kuhifadhi vyanzo vya maji.
RUWASA inawajibika kutoa miongozo na kutafuta
vyanzo vya fedha kwa ajili ya huduma za usafi wa mazingira maeneo ya vijijini.