Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

WAKALA WA MAJI NA USAFI WA MAZINGIRA VIJIJINI

"Maji Bombani"

AWESO: RUWASA SIMAMENI IMARA

AWESO: RUWASA SIMAMENI IMARA

Waziri wa Maji Mheshimiwa Jumaa Aweso (Mb) ameitaka Bodi na Menejimenti ya Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) kuwa madhubuti katika kuhakikisha huduma ya maji na usafi wa mazingira vijijini inaimarika.

Waziri Aweso amesema, changamoto ya upungufu wa watumishi kwa RUWASA isiwe sababu ya kufanya mambo yashindikane kukamilika kwa wakati bali iwe ni changamoto ambayo inabidi ipatiwe majibu ya haraka.

Wakati huo huo Aweso ameiagiza Bodi na Menejimenti ya RUWASA kuwa na mipango mizuri ya ujenzi wa miradi ya maji vijijini.